Mjane aililia Serikali

Baada ya jana Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kutolea maamuzi wananchi wanyonge waliodhulumiwa haki zao zaidi ya elfu tano na kuwataka wengine ambao hawajapata nafasi ya kukutana na wanasheria kueleza kero zao wafuate utaratibu wa kujiandikisha ili waweze kupata fursa ya kueleza kinachowasibu.

Mapema leo Rukia Said ambae ni mama mjane alitoa kilio chake kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari akidai kudhulumiwa ardhi yake na mtu aliyemtaja kwa jina la Mohamed, katika eneo la Kigamboni na kwamba hana msaada zaidi ya kupiga magoti kwa serikali imsaidie.

“Imani yangu ni kwamba serikali hii ni ya wanyonge, nimedhulumiwa ardhi yangu na Mohamed, nina vitu vyote muhimu vinavyothibitisha kwamba ile ni mali yangu, ikiwemo hati na risti ya malipo ambayo nimeyafanya kulipia ardhi, lakini leo anatokea mtu kwa sababu ana pesa na kinachoshangaza zaidi na yeye anadai kuwa na hati za ardhi yangu, huu ni utapeli mkubwa,” alisema Rukia na kuongeza;

“Ninaomba serikali inisaidie juu ya suala hili, Mkuu wa mkoa wetu ni mtu msikivu wa vilio vya wanyonge kama mimi hivyo ninaomba alitazame suala langu ili nipate haki yangu, ninaomba sana kwani sina uwezo wa kupambana na huyu bwana.”

Naye kwa upannde wake, mmoja wa watoto wa Rukia, Yahya Mbaruku alidai kushangazwa na kitendo cha mama yake kudhulumiwa ardhi jambo ambalo limesababisha waishi maisha magumu.

“Eneo hili ni lile ukivuka tu feri upande wa Kigamboni, kuna maduka na vituo vingine vya biashara, ambavyo kwa kweli vingetusaidia kusukuma maisha lakini jamaa huyo ametumia ujanja kutudhulumu haki yetu, kama alivyosema mama kwamba tunaiomba sana serikali itusaidie ili tuweze kupata haki yetu,” alisema Mbaruku.

Mpya zaidi Nzee zaidi