Serikali ya Ethiopia yatangaza hali ya tahadhari

siku mbili baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hailemariam Desalegn kutangaza kujiuzulu serikali ya nchi hiyo imetangaza ‘hali ya tahadhari’ nchini humo.

Imetoa tangazo hilo kupitia kituo chake cha televisheni yake ya taifa na kueleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kukabiliana na mfululizo wa maandamano dhidi ya serikali ambayo yanaendelea na kusababisha uharibifu.

Inaelezwa kuwa mamia ya  watu wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa ndani ya miaka mitatu ya machafuko yanayoendelea nchini humo.

Hali ya dharura ya miezi 10 ambayo ilimalizika mwaka jana imeshindwa kuzuia maandamano hayo, hususani baada ya kuachiwa huru kwa maelfu ya wafungwa wa kisiasa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia