Na Ferdinand Shayo,Longido.
Wachimbaji wa madini aina ya Ruby yanayopatikana katika Kijiji cha Mundarara Wilaya ya Longido mkoani Arusha wamelalamikia kushuka kwa bei ya ruby katika soko, kutokana na wanunuzi wachache wa madini hayo ukilinganisha na uzalishaji mkubwa wa madini hayo hali ambayo inaathiri mitaji ya wachimbaji hao pamoja na Wafanyabiashara.
Wakitoa malalamiko hayo mbele ya Manaibu Waziri wa Madini waliofika na kutembelea migodi ya Rubi na kuzungumza na wakazi wa Longido ambao ni wanufaika wa machimbo hayo wameiomba serikali iangalie upya sheria ya madini ya mwaka 2010 na kuwaruhusu wauze madini hayo bila kuyachakata ili yaweze kupata soko la uhakika .
Mwakilishi wa Wachimbaji Alais Mshao Amesema kuwa ongezeko la uchimbaji wa madini hayo yamekua yakipatikana kwa kiasi kikubwa huku wananuzi wakiwa wachache na kupelekea kupanga bei ambazo zinawaumiza wachimbaji .
Kwa upande wao Manaibu waziri wa Wizara ya Madini Dotto Biteko na Stanslaus Nyongo amesema kuwa wataangalia uwezekano wa kufanya marekebisho katika sera ya madini ili kuruhusu madini hayo kuuzwa bila kuchakatwa kutokana na hali ya madini hayo ambayo huweza kupoteza ubora iwapo hayatachakatwa vyemai suala ambalo wanalifanyia kazi.
"Maeneo Mengi tulifika wawekezaji hawana maelewano mazuri na wananchi lakini hapa imekua tofauti kwani wananchi wanafurahia wawekezaji ambao huwapatia mawe ya kugonga ambapo wanjipatia rubi ambayo inanufaisha kiuchumi" Alisema Stansalaus
Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo amesema kuwa wananchi wa Longido wamekua wakinufaika na madini hayo hivyo ni vyema kuweka utaratibu mzuri ambao Wilaya na taifa litanufaika kwa ujumla.