Serikali mkoani kilimanjaro itaanzisha kampeni ya kuiong'oa miti yote aina ya mikaratusi na kuua mizizi yake ambayo inakwenda kina kirefu ardhini na kunyonya maji mengi na hivyo kuchangia ukame na kukauka kwa vyanzo vya maji na mito iliyoko katika hifadhi ya mlima kilimanjaro..
Mkuu wa mkoa huo bi anna mghwira ametangaza uamuzi huo katika ibada ya maombi maalum ya kuliombea taifa liendelee kuwa la amani na rais john magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na kuyashirikisha madhehebu yote ya dini na waumini wake yaliyoandaliwa na ofisi yake kwenye uwanja wa mashujaa mjini moshi.
Bi mghwira amesema, miti hiyo ambayo imeota kando ya mito na vyanzo vya maji imegunduliwa kuwa ni moja ya sababu ya kukauka kwa mito na vyanzo hivyo na amewataka viongozi wa dini kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuing'oa miti hiyo kwa maelekezo yatakayotolewa na wataalam ili pia kuuhifadhi mlima k'njaro.
Askofu isaack amani wa kanisa katoliki jimbo la moshi amewataka watanzania kuwalea watoto wao kwa misingi ya maadili mema ili baadae taifa liwe na raia wema na viongozi bora ambao watapambana na rushwa, ufisadi na maovu yote katika jamii ili nchi iendelee kuwa na amani.
kiongozi wa madhehebu ya hindu bw dinesh shah amempongeza rais john magufuli kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo ya wananchi katika nyanja mbali mbali ikiwemo azma yake ya kuwa na tanzania ya viwanda bila kujali itikadi ya vyama vya siasa na madhehebu ya dini.
