Iran yakemea mashambulizi ya Marekani

Iran yakemea mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani kwa ushirikiano na Uingereza na Ufaransa nchini Syria

Tangazo lililotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Iran limekemea mashambulizi ya anga ya Marekani na washirika wake  nchini Syria kwa kusema kuwa  mashambulizi hayo yatakuwa na athari katika ukanda mzima.

Marekani inaituhumu serikali ya Assad kuendesha shambulizi la silaha za kemikali Duma wiki iliopita na kusababisha vifo vya watu  78.

Marekani na washirika wake Uingereza na Ufaransa wamendesha shambulizi hilo kama jimbu kwa jeshi la Assad kwa kushambulia raia  na silaha za kemikali.
Mpya zaidi Nzee zaidi