Jeshi la Polisi Tarime/Rorya limemkamata na kumfikisha mahakamani Mkazi wa Kijiji cha Mabera nchi jirani ya Kenya, Chacha Motongori (18) kwa tuhuma za wizi wa mtoto wa umri wa Mwaka mmoja na Nusu.
Akiongea na Wandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda Mkoa wa Kipolisi Tarime / Rorya, Hnery Mwaibambe alieleza kuwa tukio hilo lilitokea Majira ya saa 9 mchana Machi 26, mwaka huu Kata ya Sabasaba wilayani Tarime mkoani Mara.
Kamanda huyo aliongeza kuwa chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa kushindwa kulipia gharama ya matibabu ya maumivu ya mguu wake ambapo alitenda kuamua kutenda tukio hilo la kinyama.
Kamanda Mwaibambe alimtaja Mtoto aliyekuwa ameibwa na mtuhumiwa huyo kuwa ni Kisika John Mkazi wa Mtaa wa Sabasaba Kata ya Sabasaba wilayani Tarime.
“Mkazi wa kijiji cha Mabera nchi jirani ya Kenya,Chacha Mwita Motongori 18 alikamatwa na kufikishwa mahakamani Machi 26, Mwaka huu na polisi kwa tuhuma za wizi wa mtoto," alisema Mwaibambe.
Katika tukio hilo Kamanda Mwaibambe aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa njiani kuelekea Sirari mpakani mwa Tanzania na Kenya, ambapo kiini cha tukio hili ni kujipatia kipato kwani mtuhumiwa alikusudia kumficha mototo kwa muda ili apatiwe fedha kwa ajili ya matibabu ya mguu wake.
"Mama wa Mtoto Pendo Tusika (22) Mkazi wa Sabasaba aligundua kuibwa kwa mototo na kuanza harakati za kumtafuta ambapo msako ulianza mara moja na polisi kwa ushirikiano walimkamata mtuhumiwa akiwa njiani kabla hajafika maeneo husika nchi jirani ya Kenya aliko kusudia kuuza huyo Mtoto," alisema Mwaibambe.
Mwaibambe ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikano kwa vyombo vinavyo husika kama vile polisi ili watuhumiwa wa uhalifu wakamatwe na kupelekwa kunakohitajika na sheria kuchukua mkondo wake.