Idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu imezidi kuongezeka katika Mkoa wa Kigoma jambo linalosababishwa na muingiliano wa wakimbizi na raia wanaokaa karibu na kambi hizo.
Akiongea na Wandishi wa Habari Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga alisema idadi ni kubwa na inazidi mara kwa mara kutokana na kuwa mpakani na muingiliano wa wakimbizi na wenyeji.
Alisema kutokana na hali hiyo watoto hawapati mahitaji maalumu kama Chakula, Malazi na Mavazi kutokana na kutokuwa na wazazi au walezi wakuwatimizia.
Anga alisema wakimbizi wanapotoka katika kambi za wakimbizi kuweza kupata huduma za kijamii kama masoko ndio chanzo kikuu cha ongezeko hilo na kudai kiwa atahakikisha anakabiliana na wimbi hilo.
Aidha amelitaka shirika la UN kusimamia vyema ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo katika Mkoa wa Kigoma sababu ndio mkoa unaohifadhi wakimbizi wengi.