Raia wa Tanzania waishio jirani na kambi za wakimbizi mkoani Kigoma wamesema ujio wa wakimbizi hao umesababisha vitendo vya ujambazi na uhalifu kushamiri katika maeneo mbalimbali ya mkoani humo.
huo na baadhi ya watu wameuawa kwa kupigwa risasi, kujeruhiwa na kupata ulemavu wa kudumu huku mali zao zikiporwa na majambazi.
Kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya Tanzania, Umoja wa mataifa (UN) na mashirika mengine yanayoshirikiana kusaidia wakimbizi na jamii ya Kigoma inaonyesha kuwa maoni yaliyotolewa na wakimbizi na watanzania yamegusia tatizo hilo.
Afisa wa Kitengo cha Habari katika Mradi wa Pamoja Kigoma unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Didi Nafisa alithibitisha kuwepo kwa vitendo vya uporaji mali za raia hao huku wengine wakipigwa na kuachiwa ukilema wa milele.
Utafiti huo umeonyesha kuna mahusiano mabaya kati ya wakimbizi na watanzania hususan wanaoishi kwenye vijiji vinavyozunguka kambi za wakimbizi.
“Wenyeji wanalalamika kuwa kuna wakimbizi wanaotoroka kambini na kuvamia mashamba ya wananchi na kuiba mazao, kitendo hicho kimesababisha kuvuruga kabisa mahusiano baina ya pande hizo mbili, kwani wenyeji wamejikuta wakikabiliwa na njaa kutokana na mashamba yao kuvamiwa na wakimbizi na kuvuna mazao yote,” alisema Nafisa.
Licha ya kupongeza juhudi za UN na mashirika mengine ya kimataifa yanayotoa huduma za kiutu, wamelalamikia huduma mbovu za jamii zinazotolewa kwenye vijiji vinavyozunguka kambi za wakimbizi na ndani ya kambi hizo.
Mradi huo unafanya kazi katika kuboresha kilimo, nishati, uwezeshaji wa kinamama na wasichana, ujasiriamali na miradi ya maji kwa ajili ya kusaidia jamii ya wakimbizi na wananchi wanaozunguka kambi kwenye wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko.
Alisema katika kipindi cha miaka minne ya utekelezaji wa mradi Dola za Marekani milioni 55 zitatumika ambapo hadi sasa kuna Dola milioni 12 zimepatikana.
Mkoa wa Kigoma una kambi tatu za wakimbizi kutoka Burundi, Congo DRC na wachache wanatoka nchi za Rwanda na Uganda ambao wote wapo katika kambi ya Nyarugusu, Nduta na Mtendeli.