Kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza inawashikilia watu watano wilayani humo wakiwemo waganga wa jadi wawili kwa tuhuma za mauaji ya watu wanane pamoja na kuwakata wanawake sehemu za siri kwa mapanga na kisha kuziuza.
Lakini kwa kuwa ndege mjanja hunaswa ndani ya tundu bovu, hatimaye watuhumiwa hao wanaodaiwa kuwa na imani za kishirikina, wamejikuta wakiangukia mikononi mwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo.
Wakati Serikali ikipiga vita mauaji ya Vikongwe kwa imani za kishirikina, lakini bado wapo baadhi ya watu katika vijiji vya Ibongoya ëAà na Kanyerere wilayani Misungwi mkoani Mwanza, wanaendelea kufanya vitendo vya kikatili.
Kufuatia hali hiyo kamati ya ulinzi na usalama wilayani Msungwi, imefanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao, waliokuwa wakijaribu kutorokana na kisha kuwatia mbaroni, ili hatua za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake.
Watuhumiwa hao Simon Malonja, Bodoji Nchama, Charles Kasuluzu, Nchali Zacharia na Samike Kinasa, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.