Wahamiaji haramu 500 waokolewa

Tangazo lililotolewa na  kikosi cha kulinda pwani cha Italia limefahamisha kuwa wahamiaji haramu zaidi ya 500 wameokolewa katika bahari ya Mediterania.

Whamiaji hao walikuwa katika maboti ya plastiki katika bahari ya Mediterania wakiwa safarini kuelekea nchini Italia ikiwa ni moja ya hatua ya kuingia katika mataifa ya bara la  Ulaya.

Wahamiaji haramu hutumia njia hiyo hatari wakiwa na matumaini kupata maisha bora pindi watakapowasili barani Ulaya.
Mpya zaidi Nzee zaidi