WhatsApp yapiga marufuku watu hawa kuitumia



Mtandao maarufu wa WhatsApp umezuia watu walio chini ya miaka 16 kutumia mtandao huo, kwenye nchi za Umoja wa Ulaya.

Kabla ya hapo watumiaji walitakiwa kuwa na umri wa miaka 13, lakini sasa watumiaji ni lazima wawe na miaka 16 na kuendelea kulingana na utaratibu mpya wa  kulinda taarifa binafsi nchini humo.

Mtandao huo ambao unamilikiwa na mtandao mkubwa wa facebook, utawauliza watumiaji kuthibitisha umri wao watakapojisajili, kuanzia mwezi ujao mwaka huu.

Kutokana na hilo WhatsApp utakuwa mtandao wa kijamii wa tano kuhitaji umri maalum ili kuweza kuutumia, ikiwemo Facebook, Snapchat, Instagram na YouTube.