Baadhi ya wananchi wilayani Bunda wamelilalamikia Jeshi la Polisi kwa kuwanyanyasa, kuwadhulumu na kuwaomba rushwa, hali inayowafanya waishi kwa hofu.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Bunda, wananchi hao wamemwambia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kuwa vitendo hivyo vya jeshi la polisi vinasababisha wakose haki zao za msingi.
Akizungumza na wananchi hao, Lugola amewaonya askari polisi wanaotumia nafasi zao kujinufaisha na kwamba wizara yake haitavifumbia macho vitendo hivyo ,ambavyo amesema vina lenga kulichafua Jeshi la Polisi Tanzania.
