Ismail Aden Rage ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Simba, ameshangazwa na maamuzi ya klabu hiyo kushindwa kutoa elimu kinagaubaga juu ya elimu ya katiba mpya.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya baadhi ya Wanachama kuanza kutupia lawama juu ya katiba hiyo wakati wa zoezi la kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu.
Rage ameeleza kuwa yawezekana Simba wamejichanganya kwa kufanya haraka kutisha Uchaguzi kabla ya kuwapa elimu vizuri Wanachama ili waweze kuielewa vema namna katiba ilivyo.
Kiongozi huyo mstaafu anaamini suala hilo limesababisha baadhi ya wanachama kushindwa kujitokeza kuchukua fomu sanjari na ada ambayo ilikuwa imewekwa.
Kiasi cha ada ambayo ni shilingi za kitanzania laki tano kimemfanya Rage aaamini wanachama wengi kushindwa kufika makao makuu ya klabu kuchukua fomu sababu ni kubwa.
Mwanachama huyo ameeleza ifikie hatua klabu ilipaswa kuangalia na namna hali ya Mtanzania ilivyo ili kila mwenye sifa aweze kuimudu lakini kwa sasa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu kwa maana muda tayari umeshapita.
