Sister Fey mbioni kubadili Dini sababu ya Ndoa


Msanii wa filamu na muziki Bongo, Faidha Omary ‘Sister Fey’ licha ya mpenzi wake, Elias John ‘Holly Star’ kuwa mdogo kiumri ‘kiben’teni’ amefunguka kuwa yupo kwenye mpango wa kubadili dini na kuwa Mkristo ili waweze kufunga ndoa.

Akizungumza na Za Motomoto News, Sister Fey alisema kwa sasa wako kwenye mipango ya kuingia kwenye ndoa harakaharaka kwa kuwa ni mjamzito hivyo yupo radhi kubadili dini kwa sababu amependa kweli.

“Tuko kwenye mipango ya ndoa na ndani ya miezi miwili hii tutafunga ndoa, niko tayari kubadili dini, tunasubiri tu uamuzi kutoka kwa babamkwe kwamba tutafunga ndoa ya bomani au kanisani.

“Sioni shida kubadili dini au kuolewa na kijana huyo, kisa namzidi umri kwa sababu hakuna asichokijua kwenye dunia hii, nampenda na siwezi kumuacha ndiyo maana niko tayari kubadili dini nimfuate kwenye ukristo kama mzazi wake ataamua hivyo,” alisema Fey.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia