Romy Jones akizungumza na The Playlist ya Times FM amesema si kweli kwamba hawachezi nyimbo za Rich Mavoko ila ni kwamba zamu yake haijafika.
"Sidhani kama kuna shida, tumecheza ya Ommy Dimpoz, Alikiba kwanini tusicheze ya Rich Mavoko. Ukiona haijachezwa ujue mzunguko wake haujafikia, mzungumko lazima utafikia na mwisho wa siku itaendelea ile ni ya kwetu sote," amesema Romy.
Rich Mavoko alijiunga na WCB mwaka 2016 na kuweza kufanya vizuri kimuziki, mwaka huu muimbaji huyo aliondoka hapo na kuanzisha lebo yake inayokwenda kwa jina la Bilionea Kid.
Tags:
BURUDANI
