Msanii wa Bongo Flava, Diamond Platnumz amesema kuwa yeye na msanii mwenzie AliKiba walishamalizana ukafika muda wakatambua kuwa wanagombanishwa ili watu watengeneze hela.
Diamond amesema kuwa yeye na msanii huyo wameshasanuka ndio maana leo watu wanaona sisi tuko Mtwara na yeye yuko Kahama kila mtu anatafuta riziki yake.
"Nafikiri Management suala liko kwao, upande wetu sisi kama wasanii tushamaliza ikafika time tukaona kumbe tunagombanishwa ili wao watengeneze hela kupitia sisi na watengeneze content pia," Diamond Platnumz ameiambia Dizzim Online.
"Lakini tumesanuka ndio maana leo kama mnaona, sisi tuko Mtwara yeye yupo Kahama kila mtu anatafuta riziki yake, ila enzi za zamani tungekuwa wote tuko Dar es salaam tungewekeshwa katikati pale tushindanishwe tuwajazie watu hela tushasanuka," amesisitiza.
