Kesi ya Aveva na Kaburu yasogezwa mbele hadi Ijumaa


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu imeshindwa tena kuendelea na kesi inayowakabili waliokuwa  Viongozi wa Simba, Evans Aveva na Geofrey Nyange Kaburu na Zacharia Hans Poppe kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kukabidhi nyaraka za ushahidi kwa hakimu.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo mara ya mwisho upande wa mashitaka ulishindwa kutoa nyaraka hizo kwa hakumu kabla ya kuzitoa leo hali iliopelekea hakimu kuomba muda wa kuzipitia huku akisogeza mbele kesi hiyo.

 Kesi hiyo imesogezwa mbele hadi Ijumaa itakapotajwa tena  mahakamani hapo.

Aveva na Kaburu walihudhuria mahakamani hapo, awali kesi ilikuwa isikilizwe saa tano asubuhi lakini ikarudishwa hadi saa tatu asubuhi.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia