Mzee Akilimali atoa tamko hili juu ya Uchaguzi Yanga


Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali amekuja upya tena akiwapa tano Baraza la Michezo Tanzania (BMT) juu ya kuitaka Yanga ifanye uchaguzi.

Akilimali ambaye amekuwa akilipigia upatu zaidi suala la klabu hiyo kongwe kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi, ameunga mkono matamko ya BMT akisema wamefanya la maana.

Mjumbe huyo amesema ni wakati mwafaka wa Yanga kujaza nafasi haswa ya Mwenyekiti wa klabu ambayo imekuwa tupu kwa muda mrefu.

Aidha, Akilimali amefunguka Yanga haiwezi kuendelea kumlilia Yusuf Manji ambaye hajaonesha nia ya kurejea ndani ya klabu licha ya kuombwa mara nyingi.

Wakati huo watani zao wa jadi Simba jana walifanya zoezi la uchaguzi ili kuwapata viongozi wapya na mpaka siku inaelekea kumalizika, zoezi la kuhesabu kura lilikuwa linawendelea.