Na John Walter-Manyara
Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la jinsia na Watoto pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu kuanzia Mwezi Novemba 25 hadi Desemba 10 watakuwa na siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kutoa huduma mbalimbali kwa wahanga wa vitendo hivyo.
Akitoa taarifa kwa wananchi na wanafunzi katika mahafali ya Tano kwa fani mbalimbali katika chuo cha Ufundi Stadi Veta Manyara Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kutoka Dawati la Jinsia na watoto Pili Saburi amesema wiki hiyo itakuwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutoa ushauri kwa waliofanyiwa ukatili wa aina mbalimbali.
Aidha afande Pili amewasihi wahitimu huko wanapokwenda wakawe mabalozi wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo yao.
Amewaomba wananchi wafike kwa wingi katika vituo vya polisi katika wiki hiyo na wasiliogope jeshi la polisi bali waonyeshe ushirikiano katika kufichua wahalifu na vitendo vya uhalifu vinavyofanyika ili jamii ibaki salama.
Takwimu zinaonyesha kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia mkoa wa Manyara vipo kwa Asilimia 27 huku vikionekana kuongezeka kila kukicha haswa ukatili kwa wanawake na watoto.
Kutokana na hali ya Ukatili kuendelea kuwa tishio na kukatisha ndoto za wengi na wengine kupoteza maisha,serikali imeamua kuunda Kamati za Ulinzi kwa Wanawake na Watoto [MTAKUWA] kwenye kila mkoa, ambapo kwa mkoa wa Manyara ilifunguliwa rasmi na Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia wazee na watoto Dr Faustine Ndugulile Novemba 2.2018 na kuisisitiza kamati hiyo ipambane kuhakikisha inakomesha vitendo vya ukatili mkoani hapa.
Ukatili mwingine unaofanywa mkoani Manyara kwa kubuni njia mpya kila kukicha ni UKEKETAJI kwa watoto wa kike na watoto wachanga nyakati za usiku na kuacha kufanya sherehe kama walivyokuwa wakifanya wali ili wasibainike ambapo Serikali kupitia wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,jinsia wazee na Watoto imeshabaini njia hizo na kueleza kuwa imejipanga kutokomeza vitendo.
Kuanzia Januari mpaka Septemba 2017 jumla ya vitendo 41,000 vya ukatili viliripotiwa na jeshi la Polisi hapa nchini.