Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Darassa amefunguka wimbo pekee wa msanii uliomvutia zaidi wakati yupo kimya kwenye game.
Darassa ameiambia Clouds FM kuwa wimbo wa 'Iokote' uliofanywa na Maua Sama ndio uliomvutia zaidi
"Nimekaa ndani kwa mwaka mzima, Wasanii wengi wametoa ngoma zao na zimefanya vizuri, natumia fursa hii kumpongeza producer Aabbah_process kwa kufanya ngoma nzuri ya Iokote,
Watu wajue nimeanza kazi rasmi na ushindani utakuwa mkubwa," alisema Darassa.
Hivi karibuni Msanii wa Muziki, Linex naye aliutaja wimbo huo wa Maua Sama kuwa ni wimbo bora.
