Fahamu mbinu za kujiajiri

Hili ni swali ambalo litakuwa linakuja kwako kila utakapokuwa unalalamika kukosa kazi uliyoisomea. Kila mmoja wetu amezaliwa na uwezo huu wa kujiajiri.  Tumezaliwa na shauku, kiu, kufanya mambo ya hatari, uvumbuzi, akili na vitu vingine vingi ambavyo
huonyesha wazi kuwa mtu hawezi kufundishwa ujasiliamali bali uko ndani yake kiasili, kinachohitajika ni yeye  tu kujiweka katika mazingira ya  kuruhusu akili yake kutatua tatizo lililojitokeza sehemu husika.

Hapa ninakuletea mfululizo wa vitu ambavyo unapaswa kufanya ili kuiamsha hamasa ya ujasiriamali ndani yako:

 Tengeneza marafiki.
Yeyote anayetaka kuwa mjasiliamali ni lazima atengeneze marafiki wengi wenye mtazamo  chanya kama yeye. Usiwe na marafiki ambao unatofautiana nao mtazamo, watakuwa wanakukatisha tamaa kwani kwao hilo wazo wanaona haliwezekani na watakwambia huwezi.

Kauli kama hizo zitakukatisha tamaa na ukizingatia wazo lolote mwanzo huwa gumu na haliwezekani mpaka uanze kulifanyia kazi. Ndio ule msemo wa ukitembea na mwizi na wewe utakuwa mwizi unaingia hapa.

Tengeneza lengo.
Kutengeneza lengo la biashara ni hatua muhimu katika hatua za kuwa mjasiliamali.
Lengo hili uliweke katika maandishi na litakusaidia katika kuwashawishi watu kukusaidia mtaji. Mara utakapokuwa umeandika lengo la biashara unayotaka kufanya usiweke maandishi hayo kabatini,  anza kuyatafutia njia ya kuwa kitu halisi kutokana na hayo maandishi.

Na pia lengo hili litakusaidia wewe usiyumbe na kutoka katika mstari wa lengo ulilojiwekea na litakuwa ni muongozo wako.

 Jenga nidhamu.
Unapotaka kuwa mjasiliamali ni lazima utengeneze nidhamu yako ya kazi.
Kabla hujaanza kuingia hatua ya kujiajiri ili uepuke hatari ya kupoteza kila kitu jiulize kama una nidhamu ya kutosha kuingia katika hiyo shughuli.
Huwezi ukawa mjasiliamali ambaye hauheshimu hata muda wako wa kazi.

Tambua jamii inahitaji nini.
Kama unataka kuwa mjasiliamali ni lazima uwe na uwezo wa kuchemsha akili yako katika kuyasoma mazingira uliyopo yanahitaji kitu gani na wewe uje na utatuzi wake.
Lenga eneo moja ambalo unaona kweli lina uhitaji na unaweza ukaja na utatuzi wake.

Jenga wazo ambalo ni rahisi kutekeleza. 
Kama unataka kuwa mjasiliamali ni vyema ukawa umechagua eneo moja maalumu la kulitafutia ufumbuzi na ambalo  rahisi kutekelezeka. Na pia kuwa makini hilo jambo unalotaka kulifanyia kazi uwe na uzoefu nalo japo kidogo,  kwani huwezi kutibu ugonjwa usijua hata unakaa wapi.

Fanya utafiti wa wazo lako.
Ukiwa tayari umeshategeneza utatuzi juu ya jambo fulani jaribu kutafuta maoni kwa watu uliolenga kuwasaidia.  Yawezekana usiwaeleze kwa kina kuhusu wazo ulilokuja nalo lakini tafuta namna ya kulijaribu na uone wanatoa maoni gani juu ya utatuzi huo kwa kupitia huduma za bure na mitandao ya kijamii.

 Fanya bidii kuliko wengine.
Hapa lazima utambue kuwa kila mtu anaweza kuwa mjasiliamali,  lakini tofauti huja katika bidii wanayoweka katika shughuli waliyochagua. Kama umejitolea kuwa mjasiliamali ni lazima ujitoe kufanya kazi kwa bidii kuliko mtu yeyote yule.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia