Jinsi ya kuondoakana na aibu hatimaye uweze kujiamini

Wakati mwingine wanadamu tumeubwa na sura za aibu aidha kwa kujua au kwa kutokujua pia. Lakini wapo watalamu mbalimbali wa masuala ya saikolojia ambao wameleza kwa kina kuhusu namna ambavyo unaweza kuondokana na tatizo hili.

Na zifutazo ndizo njia za kuondokana na aibu:

1. Fanya kitu unachokiogopa.
Kama wewe umeumbwa na hulka hii ya aibu basi unatakiwa kuanza kitu kitakachokufanya uwe na aibu hiyo, kama huwa unaogopa kuongea kwa watu maana yake hicho ndicho unachokiogopa, hivyo ili kuweza kujinasua katika aibu hii basi unatakiwa kuanza kuzungumza mbele za watu kwa sababu hicho ndicho kitu ambacho kinakuogopesha wewe.

2. Jiweke vizuri.
Kama aibu yako imekutawala sana basi hakikisha unajiweka mwili wako na mavazi katika hali ya uzuri na nadhifu, kama ni mavazi basi vaa mavazi ambayo watu hawatakutolea sana macho yao, hii ni kwa sababu kama umevaa mavazi ya ajabu basi watu ni lazima watakuwa na wewe kukutazama, kitendo kitakachokufanya ujisikie aibu, hivyo kila wakati ili uondokane na aibu jiweke mwenyewe katika hali ya uzuri.

3. Jifunze kwa watu wengine ambao hawana aibu.
Najua katika mazingira ambayo unaishi wewe wapo baadhi ya watu huwa hawaana aibu kabisa, hivyo unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unajifunza kutoka kwao kwamba wao huwa wanafanyaje hadi kutokuwa na aibu, ikiwezekana waulize huenda wakakupa mbinu mbalimbali za kuondokana na aibu.

4. Vuta pumzi ndefu.
Kama aibu yako ni kwamba huwa unashindwa kuzungumza mbele za watu basi unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa unafanya zoezi fupi kabla ya kuanza kuzungumza na zoezi hili si jingine bali ni kuvuta pumzi ndefu kabla ya kuanza kuzungungumza mbele za watu, pia unapozungumza usipende kumuangalia mtu muda mrefu machoni pake maana atakufanya upotezee kujiamini kwako.

5.  Anza mazoezi ya kuzungungumza.
Anza kufanya mazoezi ya kuzungumza, anza kuzungumza ukiwa peke yako ili ukifika mbele za watu iwe ni kitu cha kawaida tu, mazoezi ya kuzungumza wanashauri wakati unaanza ni vyema ufanye mazoezi katika kioo ambacho kitakuonesha unazungumza. Kioo ni njia nzuri sana katika kujijengea uwezo wa kujiamini.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada, nikutakie siku njema, endelea kutembelea Muungwana blog kila wakati.

Na. Benson Chonya

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia