Kijana maarufu mtandaoni, Juma Lokole (KICHEFUCHEFU) ameshushia maneno mazito Mwanamitindo, Hamisa Mobetto kuwa ni mwizi wa waume za watu anajulikana na hiyo Kasumba anayo.
Lokole ameiambia Wasafi Tv, kuwa Mwanamitindo huyo kuwa aliwahi kuishi na Wema Sepetu nyumba moja na alimuibia Diamond.
"Hamisa Mobetto ni mwizi wa waume za watu anajulikana na hiyo Kasumba anayo miaka nenda miaka rudi, Naweza kusema nikirudisha file nyuma miaka ya nyuma kama aliweza kuishi na Wema ndani na bado akawa anatembea na Diamond baada ya hapo huyo sio mtu tena," alisema Lokole.
"Zari akawa na Diamond akaenda kuzaa na Diamond umenielewa na bado imejirudia tena kwa Tahiya yule alikuwa Boyfriend wake walikuwa wanaelekea kwenye maisha mengine pika pakua ni nusu ya mume na mke umeenda kumchukua ni mwizi tayari siwezi kumtetea angekuwa kafanyiwa yeye ningemtetea," aliongeza Lokole.
