Msanii wa Bongo Fleva, Marioo amesema kuwa siku zote anapenda kufanya vitu vinavyomzidi na ndio sababu ya kufanya vziri.
Muimbaji huyo akizungumza na Clouds 360 kupitia Clouds TV amesema kuwa anavyofanya hivyo ili watu wasichoke kazi zake.
"Kwenye muziki wangu napenda kufanya vitu vinavyozidiana kila siku na sitamani watu wazoee ninachokifanya na hata ukisikiliza uandishi wangu unaona ni tofauti, Napenda sana uandishi wangu na hata leo asubuhi niliusalimia uandishi wangu" amesema.
Marioo ameshawaandikia nyimbo wasanii kadhaa kwenye Bongo Fleva na kufanya vizuri, wasanii hao ni kama Nandy na Gigy Money.
