.

1/11/2019

Singeli imepungua kasi - Dulla Makabila


Msanii wa Muziki wa Singeli, Dulla Makabila amesema kuwa aina ya kasi ya muziki wanaoufanya imepungua kasi.

Makabila ameiambia Wasafi Tv,  kuwa watu wenye majina wamenga'nga'nia majina yao na hawataki kuwashika mkono wengine.

"Singeli imepungua kasi, yote kwasababu wenye majina wameng'ang'ania majina yao  hawataki kuwashika mkono wengine,  kuna watu wana uwezo badala ya kusema mimi na wewe tutengeneze kundi sasa kama ilivyokuwa lebo ya Wasafi, hata ukiniambia mara ya mwisho kuonana na kupiga stori na mwanamuziki wa Singeli sikumbuki lini," alisema Dulla.