Nchi ya Urusi kuzima mtandao wa Intaneti


Nchi ya Urusi inajipanga kuzima mtandao wa intaneti kwa muda, na hivyo kujitoa kwenye mawasiliano na dunia kama sehemu ya majaribio yake ya kujikinga dhidi ya mashambulio ya kimtandao.

Zoezi hilo litafanya mawasiliano baina ya raia na mashirika ya Urusi kubaki ndani ya nchi badala ya kupitia njia za kawaida za kimtandao kimataifa. Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika kabla ya Aprili Mosi mwaka huu, hata hivyo siku rasmi ya kuzimwa mtandao haijatajwa.

Vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa watoa huduma za intaneti nchini humo wanakubaliana na mabadiliko hayo lakini wanatofautiana kwenye namna gani utekelzwaji wake uwe. Wanaamini jaribio hilo lipelekea kuwepo kwa mvurugano mkubwa kwa matumizi ya mtandao ya nchi hiyo.