Rafiki leo nataka nikupe kanuni sita za kuwa na furaha kwenye maisha yako. Utafiti unaonesha watu walio na furaha kwenye maisha yao, ndio watu wanaofanya vizuri kazini, ndio watu walio na ufanisi mkubwa kwenye biashara zao. Rafiki kama huna furaha, ufanisi wako katika majukumu mbalimbali unapungua. Hizi hapa ni kanuni sita za kuwa na furaha kwenye maisha yako;
Amua kuwa na furaha.
Amua kwamba unataka kuwa na furaha na maisha yako. Amua kwamba hutaruhusu kitu chochote kikuondelee furaha yako. Ipe furaha thamani katika maisha yako. Ipe kipaumbele kwenye maisha yako.
Kuwa tayari kuviweka pembeni vitu vyote vinavyozuia wewe kuwa na furaha, na kuwa tayari kufanya au kukubali vitu vinavyokufanya huwe na furaha.
Fanya kitu unachopenda.
Watu wengi wanaofanya kitu wanachopenda wanafuraha na maisha yao. Kukipenda kitu unachofanya kunaweza kukufanya huwe na furaha. Je kitu unachofanya unakipenda au unafanya kwa sababu unatakiwa kufanya?
Utafiti unaonesha, watu wanaofanya kitu wasichopenda wanakabiliwa na magonjwa ya moyo. Watu hawa wanaenda kazini kwa sababu tu imewalazimu kwenda. Kama wangekuwa na uchaguzi wa kuchagua, basi wasingefanya kazi au biashara wanayofanya.
Rafiki kama huna furaha angalia kazi au biashara unayofanya kama unaipenda. Kama upendi unachofanya kuna vitu viwili nakushauri. Kwanza, anza kufanya unachopenda kufanya hata kwa saa moja kwa siku. Anza kufanya hata kama ni kidogo. Unaweza ukaanza kujifunza mambo mbalimbali kuhusu hicho kitu. Anza leo usisubiri kesho.
Mbili, anza kupenda unachofanya. Kama unafanya kazi ipende, kama unafanya biashara ipende. Rafiki anza kupenda kitu unachofanya kwa sababu hicho ndio kinakuingizia kipato chako cha kila siku. Unapata mahitaji yako, unasomesha watoto kupitia hicho unachofanya.
Wape watu wengine furaha.
Kuna kanuni moja ya asili inasema ” unachotoa ndio unachopata”. Kama unatoa furaha na wewe utapata furaha. Ukiwa sababu ya wengine kupata furaha, basi na wewe utapata furaha.
Rafiki yangu wape watu wengine furaha na wewe utapata furaha. Unaweza ukajitolea kwa shughuli mbalimbali za jamii. Unaweza ukaanza kwenda hosipitali ukawasalimia wagonjwa. Unaweza ukaenda kuwaona na kuwapa misaada yatima na wajane. Ukiwapa watu furaha na wewe lazima utapata furaha.
Njia nyingine ya kuwapa watu wengine furaha ni kuwapa thamani kubwa kupitia kitu unachofanya. Kama kuna kazi au biashara unafanya, basi toa thamani kubwa. Ukitoa thamani kubwa kwa watu na kuwapa kitu wanachopenda utawafanya wafurahie huduma au bidhaa unayotoa. Wakifurahi na wewe utapata furaha. Toa furaha na wewe utapata furaha.
Chagua kuwa na afya bora.
Lala vizuri. Unalala kwa saa ngapi rafiki? Tunashauriwa tulale angalau saa nane kwa siku. Jitahidi upate muda mzuri wa kulala na ulale vizuri. Kulala vizuri kutakufanya uanze siku yako ukiwa na furaha na hamasa kubwa.
Fanya mazoezi. Kufanya mazoezi kutakufanya ujisikie vizuri. Kufanya mazoezi pia kunasaidia kuepuka baadhi ya magojwa kama magonjwa ya moyo. Kufanya mazoezi kunaondoa msongo wa mawazo ( stress ). Fanya mazoezi mpaka utoke jasho.Wanashauri kufanya mazoezi angalau nusu saa kwa siku. Ukifanya mazoezi utainza siku yako vyema sana na kwa furaha.
Kula vizuri. Kula chakula bora. Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya chakula unachokula na jinsi unavyojisikia. Kula matunda na mboga za majani kwa wingi. Jitahidi ule mlo kamili kwa siku.
Cheka na epuka kuwa siriasi( seriuos) kila muda. Kucheka pia kunaondoa msongo wa mawazo kama ilivyo kufanya mazoezi. Kuwa siriasi kila muda kunaweza kukufanya ukose furaha. Hakikisha unapata muda wa kucheka na kutabasamu. Maisha ni mafupi rafiki, kwa nini huwe siriasi kila muda.
Epuka kumrizisha kila mtu.
Ijapokuwa moja ya kanuni ya kuwa na furaha ni kuwapa watu wengine furaha, lakini sio kwamba ndio utafute kumurizisha kila mtu. Kutaka kumurizisha kila mtu itakusababisha msongo wa mawazo ( stress ). Ukitaka kumufanya kila mtu afurahi itakufanya ukose furaha.
Epuka kutaka kumufanya kila mtu akupende au afurahi, kama kweli unataka kuwa na furaha. Fanya kitu kwa sababu ni dhumuni lako, fanya kitu kwa sababu unapenda kufanya, fanya kitu kwa sababu ni jukumu lako, usifanye kitu kwa sababu unataka kumuridhisha kila mtu.
Kufanya kitu ili umurizishe kila mtu, itakufanya muda mwingine kufanya vitu ambavyo hupendi kufanya. Epuka kumurizisha kila mtu rafiki yangu, utapata furaha kwenye maisha yako. Ukitaka kumurizisha kila mtu utakosa furaha kwenye maisha yako.
Kama kitu hukipendi sema hapana. Jifunze kuwa mkweli na mwaminifu. Kusema ukweli kutafanya uepuke vitu vingi na kuwa na furaha.
Kuwa chanya
Epuka kuwa hasi. Jifunze kuziona changamoto au majaribu unayopitia kama furusa za wewe kukua na kuendelea mbele. Samehe unapokosewa na omba msamaha unapokosea.
Jifunze kushukuru kwa jinsi ulivyo na kufurahia vitu ulivyonavyo. Shukuru kwa vipaji ambavyo Mungu amekupa. Hakikisha pia unazungukwa na watu chanya. Epuka watu hasi kwenye maisha yako kama kweli unataka furaha.
Kubali makosa unayofanya na jifunze kupitia makosa na endelea mbele. Elewa kwamba hakuna binadamu aliye kamilika. Binadamu wote tuna mapungufu.
Jifunze pia kuwaza mambo mazuri kuhusu kesho yako. Waza mafanikio na sio kushindwa. Waza afya na sio magonjwa.

Tags:
makala