Rage apendekeza Yanga SC wafungwe sita ili kuweka heshima Mjini


Ismail Aden Rage ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba amefunguka kuwaonea huruma Yanga SC kuelekea mechi yao dhidi ya Simba Jumamosi ya wiki hii.

Huruma hiyo ya Rage imekuja kutokana na kipigo walichokitoa jana Simba dhidi ya al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliomalizika kwa ushindi wa bao 1-0 na kusema kuwa  Simba hivi sasa imekuwa ni bora zaidi ya Yanga kwa kitakwimu.

"Nawaonea huruma watani zetu kwani Simba ya sasa ipo vizuri, ningependa kuona walau wanafungwa bao 6 pekee ili kuweka heshima hapa mjini" alisema Rage

Timu hizo zenye historia ya aina yake haswa katika soka la Tanzania zitakuwa zinakutana wikiendi ijayo huku katika mechi iliyopita zilishindwa kufungana kwa kwenda suluhu tasa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia