Simba SC kibaruani leo dhidi ya Al Ahly



Wekundu wa Msimbazi, Simba SC leo kitashuka dimbani kwa ajili ya kucheza mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Utakumbuka Simba SC waliondoka nchini January 29 na kikosi cha wachezaji 20 kuifuata timu hiyo.

Simba SC itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi AS Vita ya DR Congo kwa kulala kwa goli 5-0.

Hadi sasa Simba inashika nafasi ya tatu kwenye kundi lao ikiwa na pointi tatu sawa na AS Vita ambayo ina idadi kubwa ya magoli ya kufunga, Al Ahly inaongoza kundi ikiwa na pointi nne.