Wachinjaji na wauza nyama ya Ng'ombe walalamikia kufilisika wasimamisha huduma


Na. James Timber, mwanza

Wafanyabiashara wa nyama na wachinjaji ng'ombe jijini Mwanza wamegoma takribani siku mbili kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kufilisika kutokana na kutokuwa na mnada wa karibu na machinjio.


Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Itimbula Samson ametoa kilio hicho mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela alisema imekuwa ikiwalazimu kufuata mnada wa Nyamatala uliopo katika wilaya ya Misungwi hali inayoleta gharama kubwa katika usafirishaji wa mifugo hiyo kutokana na kuitoa wilaya moja kwenda nyingine.

Aliongeza kuwa kwakuwa wafanyabiashara wameishiwa mitaji na eneo lililopangwa kuwa mnada ambao watautumia huko mbeleni halijakamilika basi serikali iwaruhusu kutumia mnada wa mbuzi kipindi wakisubiri kuhalalishwa kwa eneo la fumagila kuwa mnada.

"Hawa wote ni wafanya biashara wa kutoka wilaya mbili Ilemela na Nyamagana na ndio hawa walikuwa katika mnada wa Nyamatala ambao upo mbali na wafanyabiashara na tangu huduma imesitishwa mnada ule haufanyi kazi tena kwa hiyo mnada ule unatumiwa sana  na wafanyabiashara wa wilaya mbili pekee," alisema.

Kwa upande wake  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela aliwaomba wafanyabiashara hao kukaa chini na kujadili swala hilo kabla hali haijawa mbaya kutokana na huduma iliyogomewa ni ya chakula na inawaathiri wengi.

Aidha Mongela aliongeza kuwa swala lililopo la kuidhinisha mnada wa fumagila sio la haraka kwasababu linasimamiwa na wizara mbalimbali hivyo wafanyabiashara waendelee kuvumilia mpaka pale utakapokamilika.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia