Takwimu mpya ugonjwa wa kifua kikuu unaendelea kuwa miongoni mwa magonjwa kumi yanayosababisha vifo vya idadi kubwa ya watu duniani licha ya kwamba ugonjwa huo unatibika.
Mwaka 2017 karibu watu milioni 1.6 walikufa kutokana na maradhi hayo ya kuambukiza, na takribani watu milioni kumi waliambukizwa, wakiwemo watoto milioni moja, wamesema wataalamu kuelekea siku ya kimataifa ya kupambana na kifua kikuu inayoadhamishwa siku ya jana.
Visa vingi zaidi vya ugonjwa wa kifua kikuu vimerikodiwa katika mataifa yanayoendelea na yanayoinukia kiuchumi. Barani Afrika zaidi ya watu nusu milioni hufariki kila mwaka kutokana na kifua kikuu hiyo ikiwa ni karibu robo ya vifo vyote vinavyosababisha na ugonjwa duniani.
