Baada ya siku ya jana kuenea video ya utupu inayodaiwa ni ya Askofu wa Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ameeleza ukweli kuhusu video hizo.
Gwajima amesema kuwa kwa mwanaume mwenye akili timamu hawezi kurekodi video ya kujamiiana yeye mwenyewe alafu mkono ukawa kama baunsa.
"Naomba kila mtu atumie akili yake ni mwanaume nani anayeweza kufanya kitendo cha kujamiiana anarekodi yeye mwenyewe alafu ukiona mkono wenyewe ni mkubwa wa baunsa sio mkono wa wangu ni mkono wa baunsa, alafu baada ya kurekodi huyo mtu anatuma alafu matokeo yake yawe haya, hakuna mtu mjinga kama huyo duniani," amesema Gwajima.
"Haiwezekani mwili uwe wa mwingine na kichwa kiwe cha mwingine, ukiangalia ni simple logic huyu mtu ameweka image mbili, image za familia ambayo niko kifua wazi nimepiga picha za kifua nyingi za namna hiyo," aliongeza Gwajima katika Mkutano wake na Waandishi wa habari jijini Dar.
Aidha Gwajima amesema kuwa waliodhani watampiga yeye na kudhani kuwa hata sema tena alisema kuwa ndio ameanza na safari hii itakuwa ni ya hatari kuliko ile na watu watajua kuwa Mungu yupo.