Klabu ya Arsenal imethibitisha kuwa mchezaji wake wa zamani Freddie Ljungberg atakuwa kocha msaidizi.
Ljungberg ataachana na nafasi yake ya U23 ili kumsaidia kocha mkuu Unai Emery. Hivyo atakua amebadilishana na nafasi na aliyekuwa kocha msaidizi Steve Bould, ambaye atachukua majukumu ya U23.