Ujerumani imeuza silaha zenye thamani yaEuro Bilioni 1 kwa nchi wanachama wa ushirika wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita vya Yemen.
Ujerumani iliruhusu mauzo hayo ya kijeshi licha ya kuwepo kwa marufuku dhidi ya kufanya hivyo, mauzo hayo yalihusisha magari ya kijeshi yenye thamani ya Euro Elfu 831.
Mwaka jana Ujerumani ilisitisha kwa muda mauzo ya silaha kwa Saudi Arabia, baada ya mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul, Uturuki.
