Abiria wa boda boda wahimizwa kuvaa kofia ngumu



Na.Amiri kilagalila-Njombe

Viongozi wa umoja wa madereva bodaboda mkoani Njombe umelitaka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuwachukulia hatua za kisheria abiria wanaokaidi kuvaa kofia ngumu pindi wanapotumia vyombo hivyo vya usafiri.

Baadhi ya abiria mjini hapo husuasani akina mama wamekuwa hawapendi kuvaa kofia ngumu wakati wakisafiri kwa kutumia bodaboda kwa kisingizio kuwa kofia hizo ni  chafu,ambapo  mwenyekiti wa umoja wa waendesha bodaboda mkoani hapo bwana Philimon Mwinuka ametoa agizo kwa madereva wa vyombo hivyo juu ya utumiaji wa kofia hizo.


“Abiria akifika wewe mpe kofia akikataa endelea na safari yako na wenzako si watakuwa mashahidi wako kwamba umempa amekataa,na ukisimamishwa na askari wewe mwambie kofia hii hapa abiria amekataa hiyo kesi sio yako,lakini hata wenzetu jeshi la polisi tushirikiane kuwachukulia hatua abiria wa aina hii”amesema Mwinuka

Baadhi ya madereva  bodaboda mjini Njombe walioshiriki mkutano ulioitishwa na uongozi wa waendesha bodaboda akiwemo George mlelwa na Nicolaus mgaya wametoa kilio chao kwa wauzaji wa pikipiki  kuhakikisha kofia zinazopendekezwa zinapatikana kwa wingi.

“serikali mtufikishie vilio vyetu kwa wanaotengeneza hizi piki piki watusaidia kututengenezea hizi kofia kubwa sio hizi ndogo”amesema George Mlelwa

Siku chache zilizopita mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Njombe Jane warioba, wakati akiongoza mafunzo ya matumizi ya namna ya kuvuka vivuko vya watembea kwa miguu alisema, kila dereva anayeendesha vyombo vya moto wakiwemo madereva wa bodaboda, wanapaswa kutii matumizi ya alama za barabarani ikiwemo kuzingatia uvaaji wa kofia ngumu hatua itakayopunguza vifo na majeruhi pindi ajali zinapotokea.

Hata hivyo mara kadhaa abiria wa bodaboda wamekuwa wakikaliliwa kugoma kuvaa kofia ngumu kwa madai ya kuwa kofia hizo ni chafu na wengine aina za usukaji wa nywele zao umekuwa ukikwamisha kofia kukaa kichwani kitu kinachotafsiriwa kujali urembo badala ya uhai.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia