Angela Merkel ana matumaini ya afya bora hadi mwisho wa muhula wake

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema leo kuwa anafahamu kwamba watu wana maswali mengi juu ya afya yake kufuatia matukio mara kadhaa ambapo alikuwa anatetemeka hadharani.

 Katika mkutano wake wa kawaida wa majira ya joto na waandishi habari mjini Berlin kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa anaweza kuendelea na kazi ofisini kwake kama kiongozi wa serikali licha ya kutetemeka kwake.

Pia kansela amezungumzia kuhusu mjadala kuhusiana na hatua ya kushangaza ya kiongozi anayemuandaa kuchukua wadhifa wake Annegret Kramp-Karrenbauer kukubali kuwa waziri wa ulinzi.

Wakosoaji wamemshutumu Kram-Karrenbauer, ambaye pia ni kiongozi wa chama cha kihifadhina cha CDU, kwa kutokuwa mkweli, wakati alionesha hapo mapema kuwa hatachukua wadhifa wa uwaziri.

Wakati huo huo, Merkel amesisitiza kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza ni lazima aendelee na makubaliano ya Brexit ambayo kifungu cha mpaka na Ireland kitaondolewa mara pande hizo mbili zitakapokubaliana kuhusu masharti ya hali ya baadaye.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia