Kaseja afunguka haya baada ya kuitwa timu ya Taifa

Kipa namba moja wa kikosi cha KMC Juma Kaseja ambaye ameitwa pia kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kitakachocheza michuano ya Chan amesema kuwa siri ya kudumu kwenye ubora wake ni nidhamu.

Tanzania itamenyana na Kenya Julai 28 uwanja wa Taifa na inatarajia kuingia kambini Julai 21.

Kaseja amesema kuwa mchezo wa mpira una kanuni zake za msingi zikifuatwa hakuna kinachoharibika.

"Wengi wanasema wanavyojiskia ila ukweli ni kwamba mpira una kanuni zake, nidhamu, juhudi na kuskiliza ndiko kumenifanya niwe hapa mpaka leo hakuna kingine," amesema Kaseja.

Makipa wengine ambao wameitwa na Kaimu Kocha, Ettiene Ndayiragije ni pamoja na Metacha Mnata wa Yanga na Aish Manula wa Simba.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia