Ufilipino: Wanafunzi 12 wafariki kwenye ajali ya gari


Wanafunzi 12 wa shule ya msingi, kati ya umri wa miaka 10 na 12, wamelifariki baada ya lori walilokuwa wakisafiria kuanguka kwenye mwamba hii leo mjini Cebu nchini Ufilipino.

Vyombo vya habari vya mitaa vya Cebu Daily News viliripoti kuwa waathrika walikuwa wakisafiri kuhudhuria tukio ambalo lilikuwa linafanyika katika mji wa Boljoon, karibu na mahali ambapo ajali hiyo ilitokea.

Afisa wa habari wa umma, Ruben Nieri, alithibitisha ajali hiyo, akisema kwamba takriban watu 20 walipelekwa hospitalini. Uchunguzi wa kubaini kilichosababisha ajali hiyo bado unaendelea.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia