Loading...

8/13/2019

Bajeti ya Simba SC msimu huu kufuru


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ amesema kuwa bajeti ya klabu hiyo katika msimu wa 2019/20 itakuwa mara mbili na nusu ya ile msimu uliopita ambayo ilikuwa ni Tsh. Bilioni 1.3 .

Akiongea na  BBC Radio amesema kuwa ameongeza bajeti hiyo ili kuifanya iwe klabu bora na kubwa zaidi barani Afrika.yenye kushindana na vilabu vikubwa barani Afrika.

“Mwaka uliopita tulitumia kama dola milioni $1 hivi, Tukanunua wachezaji wakubwa wa Kimataifa, tukatengeneza mfumo wa kusaka wachezaji ‘Scouting’ pamoja na kumpata kocha mkubwa. Bajeti yetu ya msimu uliopita itakuwa ndogo kama mara mbilina nusu hivi ukilinganisha na ya msimu huu.” amesema MO Dewji.

Akielezea sababu za uwekezaji mkubwa ndani ya klabu ya Simba, Mo Dewji amesema kuwa lengo lake kubwa ni kuhamasisha pia mashabiki kupenda timu za nyumbani zaidi kuliko zile za Ulaya.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger