Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda ametoa wito kwa taasisi,kampuni na watu binafsi kuweka matangazo na machapisho yao kwa lugha ya kiswahili.
Mmanda ambae alikuwa mgeni rasmi katika siku ya pili ya maonesho ya NANENANE kanda ya Kusini 2019, yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo, manispaa ya Lindi.
Mmanda alisema utamaduni wa kuandika matangazo na machapisho kwa lugha isiyoeleweka na wananchi wengi inasababisha wananchi hao kukosa mambo ya msingi na mazuri ya taasisi,kampuni na wafanyabishara yaliyopo kwenye mabanda yao ya maonesho.
'' Kuweka matangazo na machapisho kwa lugha za kigeni kunasababisha wananchi wengi kutofikiwa na ujumbe. Basi mkiona kuna ulazima wakutumia lugha hizo, tafsirini kwa kiswahili.
Mbali na hayo, Mmanda alitoa wito kwa mamlaka ya mapato kuwadhibiti na kuwasimamia mawakala wa mashine za kiilektroniki(EFD) wapeleke mashine kwa wateja kwa wakati na ziwe mashine halisi, imara na bora.
Mkuu huyo wa wilaya ya Mtwara alisema mamlaka hiyo hainabudi kukabiliana na upungufu wa mashine hizo kwakuwasukuma na kuwasimamia mawakala.
Mmanda alibainisha kuwa ufuatiliaji na usimamizi wakaribu utasababisha kuondoa changamoto ya upungufu wa mashine hizo na kuepuka kuuziwa mashine feki.