'Haiwezekani Wanawake kulipwa sawa na wanaume kwenye michezo'


Kumekuwa na mjadala kuhusu usawa wa malipo katika michezo kwa wanamichezo wa wanaume na wanawake, wengine wakitaka wanawake walipwe sawa na wanaume huku wengine wakipinga jambo hilo.

Kocha wa Atlanta United Frank de Boer hakubaliani na wazo la wanawake kulipwa sawa na wanaume katika michezo.

Katika mahojiano na The Guardian, Mholanzi huyo amesema haiwezekani mishahara ikawa sawa kama wanawake wanashindwa kuingiza mapato sawa na wanaume na hivyo wanatakiwa kulipwa kile wanachostahili.

“Kwangu mimi ninafikiri ni dhihaka. Kama fainali ya kombe la Dunia la wanaume wanaangalia watu milioni 500, na kwa fainali ya kombe la dunia la wanawake wanaangalia milioni 100, hiyo ni tofauti, sio sawa," amesema.

Ameendelea kwa kusema, "Na kwa hiyo wanatakiwa kulipwa wanachostahili na si pungufu, wanachostahili tu. Kama watakuwa na wingi sawa na wanaume, watapata hicho kwa sababu mapato na matangazo yataongezeka.”