Simba SC wahitaji mbeleko ya Yanga SC


Uongozi  wa Simba SC umewataka watanzania kuungana kwa sasa kwenye michezo ya Kimataifa bila kujali aina ya timu anayoshabikia.

Ofisa Habari wa Simba SC, Haji Manara amesema kuwa ni wakati wa Taifa kuungana kuzipa sapoti timu zote bila kubagua hata Yanga SC pia wanapaswa waipe sapoti Simba SC kama wao ambavyo wanazipa sapoti timu zote.

"Taifa inabidi liungane, mashabiki wa Simba, Azam FC, Simba SC lazima kwa sasa tuwe kitu kimoja, haijalishi wewe ni shabiki wa timu gani kwa sasa tupo kwenye kazi ya Taifa.

Ameendelea kwa kusema "Mafanikio ya klabu zetu zote ni kwa manufaa ya Taifa na si timu moja hivyo kikubwa ni sapoti katika kila hatua," amesema.

Kwenye michuano ya kimataifa, Yanga SC itakuwa ugenini nchini Botswana itamenyana na Township Rolles kati ya Agosti 23-25, KMC itamenyana na AS Kigali, Azam FC itamenyana na Fasil Kenema na Simba wao watakuwa nyumbani wakimenyana na UD Songo.