https://monetag.com/?ref_id=TTIb Taarifa ya Uongozi wa CCM kufuatia ajali ya Lori la Mafuta | Muungwana BLOG

Taarifa ya Uongozi wa CCM kufuatia ajali ya Lori la Mafuta


Uongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM, umepokea kwa mshtuko taarifa ya ajali ya lori la mafuta iliyotokea huko Msamvu Morogoro.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa rai yao kwa Jeshi la Polisi na Zimamoto ni kuendelea kutoa elimu na kusimamia utii wa sheria.

"Uongozi wa CCM umepokea kwa mshtuko taarifa za ajali ya lori huko Msamvu Morogoro ambayo imegharimu maisha ya watanzania. Rai yetu kwa Jeshi la Polisi na Zimamoto ni kuendelea kutoa elimu na kusimamia utii wa sheria. Tunatoa pole kwa wafiwa na majeruhi kupona haraka," ameandika Polepole.

Watu wengi wamekufa kwa moto wakati wakijaribu kuchota mafuta baada ya gari la kubebea mafuta kupata ajali mjini Morogoro. Mashuhuda wanadai moto ulianza baada ya mtu mmoja kuchomoa battery ya gari na kusababisha cheche