Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amemuomba msamaha Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam kwa kile alichoeleza kuwa siku za hivi karibuni yametokea mambo mengi.
Waziri huyu wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amefunga safari hadi Ikulu Dar es Salaam kuonana na Rais Magufuli ambapo leo ndipo wamekutana na kuzungumza.
"Nimekuja kumuona kwa sababu mnajua mambo yaliyopita, hapa katikati kumetokea mambo mengi. Mimi kama mtoto wa CCM nimeona ni vizuri nije niongee na Baba yangu na nina shukuru amenisamehe na amenipa ushauri," amesema.
Kwa upande wake Rais Magufuli amesema, "Na mimi nimeshamsamehe kwa dhati, Nape amekuwa akiandika hata meseji nyingi hata usiku wa manane akiomba msamaha, unamuona kabisa huyu mtu anaomba msamaha".
