Pambano la Andy Ruiz Jr na Anthony Joshua kutanguliwa na mapambano ya Wanawake


Katika pambano la marudiano kati ya Andy Ruiz Jr na Anthony Joshua pambano la kuwania mikanda ya WBA, WBO na IBF litakalofanyika nchini Saudi Arabia Disemba 7 mwaka hu, Anthony Joshua ameibuka na kudai inawezekana na kuwa na pambano la wanawake katika mapambano ya utangulizi.

Akiongea na kituo cha BBC 5 amesema wanaangalia uwezekano wa kuweka wanawake katika mapambano ya utangulizi.

"Toka kutangazwe kwa pambano hili kufanyikia nchi humo shirika la haki za kibinadamu Amnesty International limeonyesha rekodi mbaya ya nchi hiyo katika ukandamizaji wa haki za binadam," alisema.

"Wanawake nchini humo waliruhusiwa kuendesha magari kwa mara ya kwanza mwaka 2018 ila bado wanahitaji ruhusa kutoka kwa wanaume zao ili wapate kusafiri ama kumiliki pasi ya kusafiria jambo ambalo linaonekana ni ukiukwaji wa haki za kibinaadamu,".

Nchi hiyo inayotegemea uchumi wake toka kwenye mafuta inaonekana kuwekeza katika michezo, sanaa na utalii ili kuweza ongeza kuacha tegemea sehemu moja tu.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia