Mchezaji wa zamani wa Malindi, timu ya taifa ya Zanzibar na Taifa Stars Bw. Abdallah Hussen Al'bakkry 'Abdul Malaika' amefariki akiwa Marekani.
Ni mchezaji aliyefunga bao dhidi ya Pamba ya Mwanza uwanja wa Kirumba mwaka 1988 na kuifanya Malindi kuchukua ubingwa wa Tanzania kwa mara ya kwanza.