Watu saba wakamatwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya


Jeshi la polisi Mkoani Mwanza limewakamata watu saba kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Miongoni mwa waliokamatwa katika operesheni hiyo maalumu ni pamoja na Elizabeth Lucas na Hamza Haruna waliokutwa na Gram 10 za dawa za kulevya aina ya Heroine.

Wengine waliotajwa na Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Jumanne Muliro ni pamoja na Herena Nagambona ,Yahya Haruna, Shaban Said, Nestory Moses na Zainab Zakaria waliokamatwa na Kg 30 za dawa za kulevya aina ya Bangi.