Mshtakiwa Dominick Shayo mwenye umri wa miaka 58 anayekabiliwa na shtaka la kumtelekeza Mkewe na Watoto 3, amedai hakuitelekeza Familia isipokua aliona ni bora atoweke nyumbani kwake baada ya Mwanae wa kiume kumtishia kumuua kwa panga.
"Mheshimiwa Hakimu yaani huyo Mke wangu, wale Watoto wote wapo upande wake, ikitokea tumepishana kidogo tu na Mke wangu basi wao huwa upande wa Mama yao, kitu ambacho kimekuwa kikiniumiza na kuniweka katika mawazo sana"
Shayo ambaye ni Dereva wa TRA amedai hayo katika Mahakama ya Mwanzo Jijini Mbeya mbele ya Hakimu Diana Manase ambapo amesema kinachompa simanzi zaidi ni kitendo cha Mke wake kuwakatisha masomo Watoto na kuendelea kuwapandikiza chuki zisizokuwa na faida na matokeo yake ni kubomoa na kuleka mpasuko wa kifamilia.
"Hata ikitokea nikastaafu sina hata Mtoto mmoja ninayeweza kujivunia kuwa ni msomi zaidi ya kuendelea kunitegemea mimi kwa kila kitu" amesema.
