Loading...

10/06/2019

Bil. 93.8 zatumika kuimarisha miundombinu katika shule 588 za msingi na sekondari

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amewapongeza waandishi wa habari kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhabarisha Wananchi kuhusu masuala ya sekta ya elimu na Serikali kwa ujumla.

Dkt. Leonard Akwilapo ameyasema hayo wakati wa kikao kati ya wahariri wa vyombo vya mbalimbali vya habari na wizara hiyo ambapo alielezea  kiwango cha elimu nchini na kusema kinaendelea vizuri na hatua mbalimbali zinafanyika kuiboresha sekta ya elimu.


Ameongeza kuwa Dira ya wizara ni kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa.

Dkt. Akwilapo ameongeza kuwa jumla ya shilingi  Bil. 93.8 zimetumika kuimarisha miundombinu katika shule 588 za msingi na sekondari zikiwemo shule kongwe. ambapo serikali imeongeza mikopo ya elimu ya juu kutoka Tzs Bil. 424.7 mwaka 2018/2019 hadi Tzs Bil. 450 mwaka 2019/2020.

Akielezea kuhusu  makusanyo ya madeni ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu amesema yameongezeka kutoka Tzs Bil. 21.1
mwaka 2014/2015 hadi Tzs Bil. 183.2 mwaka 2018/2019 ambapo wizara inafanya mapitio ya sera ya elimu ya mwaka 2014 ili kuifanyia maboresho na kuendana na wakati.

Amewaasa viongozi wa sekta ya elimu kushirikiana na waandishi wa habari kwa uwazi ili wananchi wapate taarifa za sekta ya elimu zenye usahihi na kwa wakati.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger