Breaking News: Michael Wambura aachiwa huru

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu (TFF), Michael Wambura ameachiwa huru na mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam.

Wambura ameachiwa huru baada ya kuingia makubaliano na upande wa Jamhuri kulipa zaidi ya TSh milioni 100 ambazo alijipatia isivyo halali.

Ufafanuzi uliotolewa na hakimu mkazi kisutu ni kwamba Wambura atalipa fedha hizo kwa awamu tano na  kwa masharti ya kutofanya makosa yeyote kwa kipindi cha miezi 12, ambapo leo amelipa Tsh milioni 20.

Hii imekuja baada ya Wambura kumuandikia barua Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP)kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alishauri kwa wale wote wenye kesi za uhujumu uchumi kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yanayomkabili mahakamani hapo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia